Header

HIJA KISHOMBERWA

Every last Sunday of the Month of JanuaryKishomberwa yawa Nafasi ya Hija

Baada ya Yohana Maria Muzeeyi pamoja na wenzake 21 kutangazwa watakatifu, Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa alifanya ibada rasmi ya hija ya kumtambulisha Mtakatifu huyo tarehe 3 Juni 1966. Ibada hii ilifanyika kwenye kilima cha Kishomberwa karibu na shamba alipozaliwa kwani sehemu yake ya kuzaliwa ilishamilikiwa na mtu mwingine. Tangu hapo, Hija Kijimbo kwa Mtakatifu huyu zimekuwa zikifanyika kila mwaka kwa kuzingatia tarehe hiyo.

Hata viongozi wa ngazi za juu za Kanisa wamekuwa wakifika Kishomberwa kufanya Hija. Mfano, mwaka 1986, Balozi wa Baba Mtakatifu, Askofu Mkuu Vicenzo Moreni, katika ziara yake Jimboni Bukoba alifika kuhiji Kishomberwa kwa Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi. Mwingine ni Askofu Mstaafu Adrian Ddungu wa Masaka, Uganda ambaye katika matembezi yake Jimboni Bukoba alifika Kishomberwa kuhiji akisindikizwa na mwenyeji wake Askofu Nestor Timanywa. Aidha, Askofu Yohana Batista anayeliongoza jimbo la Masaka kwa sasa hufika Kishomberwa kuhiji mara kwa mara. Kila wamalizapo Ibada ya Hija kwenye kijiji jirani cha Kilaiya, ambako ndiko wanakomheshimia Mtakatifu huyu, huwaongoza waamini wake hadi Kishomberwa alikozaliwa Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi.

Baada ya kuona kwamba eneo la kilimani anakoheshimiwa Mtakatifu huyu ni dogo na haliruhusu waamini wengi kufuata ibada ya hija vizuri, uongozi wa jimbo uliamua kununua eneo jingine kubwa zaidi lililoko chini ya kilima cha Kishomberwa ambalo ni sehemu ya shamba alimozaliwa na kukulia Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi. Kwa sasa, hija za kijimbo zinafanyika katika eneno hili ambalo ni pana zaidi.

Aidha, ili kuwawezesha waamini wengi kuhudhuria hija za kila mwaka kijimbo, tarehe ya hija ilibadilishwa na kuwa Jumapili ya mwisho ya mwezi Januari ambayo mara nyingi hukaribia tarehe 27 Januari – tarehe ya kuuawa kishahidi Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi.

Na Pd. Thomas R. KagumisaTumshukuru Mungu kwa Kutujalia Mt. Yohana Maria Muzeeyi

Askofu Nestori Timanywa, Jimbo Katoliki la Bukoba

Heko waamini na watu wote wenye mapenzi mema. Tumshukuru Mungu kwa kutujalia Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi, mmoja wa mashahidi ishirini na wawili wa Uganda. Ndiye Mtakatifu wa kwanza Mtanzania.

Ili kuelewa mazingira alimozaliwa, kukulia, kupata imani na hatimaye kufia ushahidi, tukumbuke kuwa zilikuwa nyakati za mataifa ya Ulaya kuvamia Afrika ili kujipatia nafasi za kufanyia biashara. Uvamizi huu ulijulikana kihistoria kama "Scamble and Partition of Africa." Katika mkutano wa nchi za Ulaya uliofanyika mjini Berlini, Ujerumani, Desemba 1884-1885, "Uvamizi wa Afrika" ulihalalishwa na kurasimishwa. Tanganyika iliangukia kuwa chini ya himaya ya Wajerumani na Uganda chini ya himaya ya Waingereza. Lakini mipaka kati ya nchi hizi mbili haikuwa wazi na ya uhakika kama ilivyo saasa.

Mipaka ya tawala za jadi ilifuata vitenganishi asilia kama vile mito, misitu, mabonde, maziwa na milima. Hivyo, himaya ya Kabaka ilienea kusini hadi mto Kagera kama kitenganishi asilia. Ndiyo maana kata ya Minziro alimozaliwa Yohana Maria muzeeyi ilihesabika kama sehemu ya himaya ya Kabaka.

Mnamo mwaka 1890, mpaka kati ya Uganda, chini ya Waingereza, na Tanganyika chini ya Wajerumani ulisimikwa kufuata nyuzi 1 (1̊) kusini mwa Ikweta. Kwa mantiki hii mahali alipozaliwa Yohane Maria Muzeeyi paliangukia Tanganyika ambayo sasa ni Tanzania, na pamebaki hivyo hadi sasa. Hili ndilo "kosa lenye heri!" Kama si wakoloni kugawa maeneo kwa faida yao ya biashara na kutawala, Yohane Maria Muzeeyi angebaki ni Mtakatifu wa Uganda. Lakini imethibitishwa na Monsinyori Timoteo Ssemogerere aliyekuwa msimamizi wa mchakato wa kuwatangaza mashahidi wa Uganda kuwa watakatifu, kwamba Yohana Maria Muzeeyi alizaliwa Kishomberwa ya Tanzania. Ama kweli, "Utajiri, hekima na elimu ya Mungu ni kuu mno! Huruma zake hazichunguziki na njia zake hazieleweki" (War 11:33).

Tunapowaleteeni historia ya Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi, tunapenda kukariri maneno aliyosema Padre Mapeera mara baada ya kuwabatiza wakristo hao shujaa tarehe 1 Novemba 1885 katika sikukuu ya Watakatifu wote, akisema, " Tunahisi kwamba nchi ya Uganda itapata matatizo mengi. Hadi kufikia sikukuu nyingine ya watakatifu wote, baadhi ya Wakristo wapya, atakuwa wamekwisha kumwaga damu yao kwa ajili ya dini zao. Ndio mashahidi wa mbingni watakaopokelewa huko mara moja na watakuwa ni waombezi wetu. Damu yao itamwagwa juu ya ardhi hii ili iweze kuzaa wakristo wengi sana. Yesu kristo atashinda na shetanni atashindwa.Watu wengi sana wataokolewa".

Maisha ya Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi yanaonesha wazi kuwa ushahidi wa kumwaga damu ni kilele tu cha ushahidi wa kuvuja jasho yaani ushahidi wa maisha. Alipambana na matatizo mengi sana dhidi ya imani na maisha safi ya kikristo, hatimaye akawa mshindi hata ilipomdai kutolea maisha yake. Nao utabiri wa Padre Mapeera umetimia, Kristo ameshinda na shetani ameshindwa. Watu wengi sana wanaokolewa. Sisi tulio wazao na warithi wa imani kuu ya Mashahidi wa Uganda, hususan Mt. Yohana Maria Muzeeyi tunayo heshima na wajibu wa kuiga mfano wake. Tumfahamu uli tumuige.

Nawakaribisheni kwenye hija yetu ya kila mwaka Kituoni kishomberwa – Minziro, Jimbo Katoliki la Bukoba.Yohana Maria Muzeeyi Ndiye Mtanzania Pekee Kutangazwa Mtakatifu

Na Askofu Methodius Kilaini (Askofu Msaidizi, Jimbo Katoliki la Bukoba)

Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi ni mmojawapo kati ya Mashahidi ishirini na wawili wa Uganda waliotangazwa rasmi na Papa Paulo VI tarehe 18 Oktoba 1964, katika Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikano kama watakatifu wa kanisa. Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi ndiye Mtakaifu pekee Mtanzania aliyetangazwa rasmi kuwa Mtakatifu na kanisa na hivyo ana maana kubwa sana kwa Tanzania.

Katika hija ya hapo Namugongo – Kampala, nchini Uganda, mahali ambapo kiongozi wa vijana mashahidi, Kalori Lwanga, aliuawa kwa kuchomwa moto, Mhashamu Askofu Mkuu Cyprian Lwanga wa Jimbo Kuu la Kampala aliwatangazia mahujaji kwamba Yohana Maria Muzeeyi ni shahidi kutoka Tanzania na akamweleza kama kiungo cha damu kati ya Tanzania na Uganda.

Tunamshukuru sana Baba Askofu Nestor Timanywa wa Jimbo la Bukoba ambaye amefanya juhudi nyingi kukiendeleza kituo cha hija cha Kishomberwa alipozaliwa Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi na kufungua parokia mpya ya Minziro ili kukipa umuhimu na uangalizi. Tuna jukumu kubwa la kulinda urithi huu wa kumbukumbu ya shujaa wetu wa imani.

Nachukua fursa hii kumshukuru Padre Thomas Rutashubanyuma ambaye amekamilisha utafiti juu ya shahidi huyu shujaa kiasi kwamba sasa tunamjua zaidi na tunaweza kufuasa katika nyayo zake. Tunawashukuru vilevile kwa kutupa kimaandishi utaratibu wa ibada ya hija inayofanyika kila mwaka katika kituo hiki cha Kishomberwa. Kijitabu hiki kitasaidia sana kumjua Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi, kurahisisha hija katika kituo cha Kishomberwa na kueneza habari zake kwa watu wenye mapenzi mema.

Tukirudia tamko la Baba Askofu Nestor Timanywa, tunawakaribisha waamini wote kutoka sehemu zote za Tanzania, Afrika Mashariki, Afrika na dunia nzima kuja kushuhudia makuu ya Mungu hapa Kishomberwa kupitia kwa shahidi wake, Yohana Maria Muzeeyi wakati wowote lakini hasa Jumapili ya mwisho ya mwezi Januari, ikikumbukwa kwamba alifariki tarehe 27 Januari 1887.

Mtakatifu Yohana Maria Muzeeyi na mashidi wote wa Uganda, Mtuombee.

Baadhi ya Nyimbo Wakati wa HijaRugaba Singa
Rugaba Singa batutunge amani, ga Abajulizi balumuna baitu,
Tugonze Yezu okukira byona, kukira byona.

1. Bakristu ija tusiime Omukama, akatendeka balumuna baitu
Abajulizi yabaha ekitinwa, owe Omwigulu.

2. Yesu akasinga yabaiya omu lufu, akabaimukya yabeta ati mwije
Bamuhulira, bayetaba bwangu, bamuhondera.

3. Nirwo bakwetwe Omukama wensi, yabarwanisa, bayanga kutina
Yalembalemba, bayanga kulembwa, bagonza Yezu.

4. Aga Matiasi bagutula gombi, n'emikono ye baleta omuliro
Omumaishoge, babimwokezaho, yaleba kushai.

5. Kalori Lwanga bati tukutunge, yayanga ebyensi, yasima ebyeiguru
Yesiga Yezu yamushaba amani, yafa ali manzi.

6. Abandi bona bakaitwa omuliro, baba kitambo Ky' Omukama Mungu
Emyoyo yabo yatungwa omwigulu, ebyera bingi.

7. Mwemezi waitu Mutonzi wa byona, niwe oba mperwa y'Abatakatifu
Oli kasinga, bakuhaisirize, ebiro byona.


Iii Tushemelerwe

Iii iii tushemelerwe, tushandukire muno Abajulizi
Iii iii tuhaisirize, Abajulizi baitu aba Uganda,


1. Tuhaisirize, Kalori Lwanga, niwe yakuliraga abajulizi,
Ayayemeire akagumisa, Abajulizi baitu aba Uganda.

2. Tuhaisirize Balikuddembe, ayabandize kufa omukubanza,
Omushaija emanzi, omwesigwa kwo, batushabire tugye owa Mungu.

3. Tuhaisirize na Ta Muzeeyi, omujulizi waitu emanzi yaitu,
Ekyaro omwabo ni Minziro, hoya muno singiza na akanyahwera.

4. Tuhaisirize na Ssebugwawo, omujulizi ondijo ayahondeire,
Na Ponsiano, Andrea Kaggwa, Atananzio niwe Badzekuketta.

5. Tuhaisirize Gonzaga Gonza, Mulumba Mawagali Banabakintu,
Buzabalyawo, Bruno Ludigo, Kibuka Akileo na Kirigwaijo.

6. Tuhaisirize omwana Kizito, akaba ali muto kukira boona,
Bakamulenga emihanda yona, kyonka yasinga yafera edini ye.

7. Tuhaisirize, Mbaga Tuzinde, Mukasa Kiriwawamvu na Ta Gyavira,
Na abandi bona tubasingize, Abajulizi baitu aba Uganda.


For more information contact:
The Parish Priest, Minziro Parish
Cell: +255 787 157 393
E-mail: revoijumba@yahoo.com

Contact Information
Bishop's House Ntungamo,
P.O.Box Private Bag,
Bukoba, Tanzania.
Tel. & Fax. 028 - 2220746
Office: Tel. 028 - 2220194
E-mail: b.officebk@yahoo.com
Website: www.bukobadiocese.co.tz
© Bukoba Catholic Diocese 2023
Find us on
Facebook: Bukoba Catholic Diocese
Twitter:  @bcdcatholic